Idadi ya watu waliokufa katika ajali ya mashua iliyotokea magharibi mwa
Uganda imefikia 108. Kamishna anayeshughulikia mambo ya wakimbizi katika wizara ya misaada, kukabiliana na maafa na kuhudumia wakimbizi ya Uganda Bw. David Kazungu, amesema miili 108 ilitolewa kutoka Ziwa Albert jana mchana. Abiria wengi walikuwa ni wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waliokuwa wanarudi nyumbani.
Bw. Kazungu ameongeza kuwa idadi ya jumla ya watu waliokuwepo mashua hiyo bado haijulikani, na watu 45 wamenusurika katika ajali hiyo. Amesema wanaendelea kutafuta miili, lakini uwezekano wa kupata watu wengine walionusurika ni mdogo.
No comments:
Post a Comment