“Unajua mimi ni binadamu na ili nitulie na kujiepusha na majanga, ni vyema kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu, anayenijali mimi na kazi yangu hapo nitasimama na kusema kwamba nimepata sehemu ya kutulia na kuanza maisha mapya ya uhusiano na ndoa,” anasema Lulu.
Hata hivyo anasema yeye na mchumba huyo (ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake) wana mikakati mingi katika kuyafikia maisha ya uhusiano yaliyo wazi na yenye baraka za wazazi.
“Siwezi kukutajia jina kwa sasa itafika wakati atajulikana tu, hata hivyo bado hatujafikia hatua muhimu ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa wazazi na masuala ya mahari na ndoa. Vitu kama hivi vitafanyika baadaye mwaka huu, hata hivyo wazazi wangu sidhani kama watakuwa na pingamizi katika hili kwani mimi ni mtoto wa kike na nimekua sasa,” anasema.
Kuhusu Mama Kanumba Lulu anasema: “Huyu ni mama yangu hana tofauti na mama Lulu hivyo anajua kila kitu na amenipa baraka zake zote, yaliyopita si ndwele kinachotakiwa ni kuganga yajayo, namshukuru mama kwani amenionyesha upendo wa kweli na kunishauri katika maisha, bila yeye nisingekuwa na ujasiri nilionao sasa.

No comments:
Post a Comment