Kijana Zakaria Ulaya amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya 
Tabora mjini akituhumiwa 
kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa Shule ya 
msingi Gongoni tukio ambalo lilifanyika huko kata ya Ipuli manispaa ya 
Tabora,akisomewa maelezo ya kosa Zakaria amekana kuhusika na tukio 
hilo,hata hivyo amerjeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutekeleza 
masharti ya dhamana ambapo walihitajika watu wawili ambao wangeweza 
kumdhamini kwa fedha zenye thamani ya shilingi milioni tatu kila 
mmoja.Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 12 March mwaka huu.
 
 

 
 
No comments:
Post a Comment