Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, January 14, 2014
BOMU LINGINE LALIPUKA..................HATARI...........
Shambulizi la kujitoa mhanga ...........
Jeshi la Serikali limekuwa likipambana na Boko Haram imekuwa vigumu kuliangamiza
Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari moja limelipuka na kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa.
Majeruhi walionekana wakitoroka eneo la shambulizi ambalo lilikuwa na uharibifu mkubwa, huku wanajeshi wakifyatua risasi hewani.
Duru zinaarifu kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga ndiye aliyesababaisha shambulizi hilo lililotokea
karibu na soko rasmi huko Nigeria.Duru zinasema kuwa huenda shambulizi lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram, limekuwa likihusika na mashambulizi kadha wa kadha katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha kundi hilo.
Boko Haram linatumia ghasia na mauaji kushinikiza serikali kuidhinisha sheria za kiisilamu kutumika Kaskazini mwa Nigeria.
Jeshi limethibitisha kutokea kwa mlipuko huo, lakini halikuweza kueleza idadi ya walioathirika.
Mtu mmoja aliyeshuhudia shambulizi hilo amesema ameona miili ya baadhi ya waliouawa kwenye shambulizi hilo ikiwa imetapakaa ardhini.
Gari la pili lililokuwa limeegeshwa kando ya gari lililolipuka liliteketea kutokana na mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment