Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Saturday, June 11, 2016
Bandari ya Libya yakombolewa kutoka kwa IS
Image caption
Sirte
Vikosi vya Libya vinavyoegemea serikali ya muungano mjini Tripoli vinasema kuwa vimeichukua bandari ya mji wa sirte, kufuatia makabiliano makali baina yao na wapiganaji wa Islamic state.
Msemaji wa kikosi hicho jenerali Muhammad al-Ghusri anasema viongozi wakuu wa Islamic State wametorokea jangwani, akiongeza kuwa wapiganaji wengi wa Islamic State wamezingirwa mjini Sirte na kuwa makabiliano yanaendelea.
Image copyright
REUTERS
Image caption
Wanajeshi wanaounga mkono serikal ya Umoja wa Matifa nchini Libya waingia Sirte
Vita vya kuukomboa mji wa Sirte kutoka kwa wapiganaji hao ikiwa ndio ngome yao muhimu nje ya Iraq na Syria vilianza mwezi uliopita.
Vikosi hivyo vinavyounga mkono serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli vilianza harakati za kuukomboa mji huo mwezi uliopita.
Mbatia asema jambo kuhusu Naibu Spika Dr. Tulia Akson
"Nina miaka 25 niko kwenye siasa.Wakati tunapambana kwa ajili ya Watanzania miaka hiyo yote hatukuwahi kuwa na posho.Kipindi hicho kina Tulia walikuwa shule ya msingi" Source: Mh Mbati James
HILI NI TAMKO LA AL-SHABAB
Image copyright
AP
Image caption
wapiganajia wa kundi la Kigaidi la al-Shabab
Kundi la wanamgambo nchini Somalia, al-Shabab, wanasema wamewaua watu watatu kwa kuwapiga risasi na kumchinja shingo mwingine, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa majasusi wa mashirika ya ujasusi ya Kenya na Marekani.
Mauaji hayo yalitekelezwa mbele ya umati wa watu katika mkoa wa Bakool.
Image copyright
Image caption
Ahmed Godan
Kulingana na taarifa ya radio ya al-Shabaab, mwanamume mmoja aliyeuawa ni Mohamed Aden Nur, ambaye anashutumiwa kuwa aliwasaidia Wamarekani kumuua kiongozi wa kundi hilo Ahmed Godane.
Mwingine aliyepigwa risasi anadaiwa kuwa alisaidia Wamarekani kumuua Adnan Garaar, anayeaminika kuongoza shambulio la kigaidi katika duka la Westgate nchini Kenya mwaka wa 2013
MAOMBOLEZO YA MSIBA WA BONDIA ALI YASHIKA KASI...
Image copyright
Bill Clinton
Ibada ya ukumbusho iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.
Image copyright
GETTY
Image caption
Baadhi ya mabondia na muigizaji Will Smith waliohudhuria hafla hiyo.
Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.
Image copyright
AP
Image caption
Umati wa watu waliohudhuria hafla ya kumbukumbu hiyo
Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake.
Image copyright
REUTERS
Image caption
Mkewe Muhammad Ali
Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.
Image copyright
REUTERS
Image caption
Msafara wa mwili wa Muhammad Ali kabla ya kuzikwa nyumbani Louisvile Kentucky siku ya Ijumaa
Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.
Older Posts
Home
Subscribe to:
Posts (Atom)