NGASSA: “Diamond ni rafiki yangu, lakini mpira huu nitampelekea
Wema kwa kuwa ni shemeji yangu na tunaheshimiana sana,” alisema Ngassa
na kuongeza: Mrisho Ngassa wa Yanga, jana alifanikiwa kufunga mabao
matatu ‘hat trick’ katika mechi dhidi ya JKT Ruvu, lakini ametoa kali
kwa kusema kuwa mpira aliokabidhiwa kwa kufunga mabao hayo, anaupeleka
kwa shemeji yake, Wema Sepetu. Akizungumza baada
ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara
iliyomalizika kwa timu yake kupata ushindi wa mabao 5-1, Ngassa huku
akionyesha kuwa na furaha, alisema kuwa mpira huo umeongeza hamasa kwa
timu yake, lakini moja kwa moja atampelekea Wema ambaye ni mpenzi wa
mwanamuziki Diamond. “Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa na timu yetu,
sisi tutapigana mpaka dakika ya mwisho ili kuhakikisha tunashinda mechi
zote. Wakati mwingine tunashindwa kucheza vizuri mikoani kwa kuwa
viwanja vinakuwa havina ubora mzuri.” Yanga imepata ushindi wa mabao 5-1
dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuamsha mbio za ubingwa dhidi ya Azam ambao
ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara, lakini kipa Juma Kaseja na mshambuliaji
raia wa Uganda, Emmanuel Okwi hawakuwepo kwenye kikosi kilichoanza wala
kwenye benchi. -
No comments:
Post a Comment