Jaji Liundi, Hashim Saggaf wafariki dunia
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Jaji, Georgeb Liundi nyumbani kwake Keko jijini Dar es Salaam jana. Jaji huyo anatarajiwa kuzikwa kwenye makaburi ya Chang'ombe keshokutwa. Picha na na Silvan Kiwale.
Taifa limepoteza watu wawili mashuhuri. Hao ni Msajili wa Kwanza wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji George Liundi (78) na Mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini, Hashim Saggaf.
Jaji Liundi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana alipokuwa akipelekwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu wakati Saggaf, ambaye alikuwa Diwani wa Mtafukoge, Dar es Salaam alifariki jana saa nne asubuhi kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Saggaf alizikwa jana kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na mazishi ya Jaji Liundi yamepangwa kufanyika keshokutwa.
Jaji Liundi
Wakati akiianza kazi hiyo, mfumo wa vyama vingi ulikuwa hauna nguvu, huku vyama vya siasa vikiwa vichache na kikubwa cha upinzani kilikuwa NCCR-Mageuzi.
Alisema alikuwa yu mtu mwenye afya njema, lakini siku tatu zilizopita alikuwa akilalamika zaidi kuumwa mgongo.
“Afya yake ilikuwa nzuri licha ya kuwa alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu (BP), alikuwa akipatiwa matibabu kila alipokuwa akijisikia vibaya, kifupi alikuwa katika hali nzuri,” alisema Taji na kuongeza:
“Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilimpeleka kwa daktari wake na kupatiwa matibabu. Jumapili (juzi) aliamka akiwa na afya nzuri,” alisema Taji.
Alisema hali ya Liundi ilibadilika ghafla usiku wa kuamkia jana, huku akiwa analalamika kuumwa mgongo... “Niliamua kumpeleka TMJ lakini tukiwa njiani, alifariki dunia.”
Taji alisema sasa wanasubiri ripoti ya madaktari, lakini wanaamini ugonjwa uliyomuua baba yao ni malaria kali. Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.


No comments:
Post a Comment