Tukio hilo limetokea leo majira
ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa
kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye
viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa
Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Inspector
Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji,
kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha
mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.
Inspector
Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti)
wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na
kubaki mtupu akiwa ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
Ushawishi ukiendelea.
Mahabusu
Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu
katu waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza
kuzungumza na waandishi wa Habari.
Wananchi wakiwa wamefurika viwanja vya mahakama.
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
No comments:
Post a Comment