Risasi ilimuingia kichwani mtoto huyu....
Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda mjini Mombasa pwani ya
Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili na kuwapiga risasi
waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo amefikishwa Nairobi mwa matibabu
maalum.
Madaktari wanasema kuwa ubongo wa mtoto huyo umefura na kwamba risasi iko
upande wa kulia wa ubongo wenyewe. Upasuaji unatarajiwa kufanywa baada ya wiki
mbili.
Inaarifiwa risasi aliyomuingia kichwani Cyprian ni risasi iliyomuua mamake kupitia kwa kifua chake na kuishia katika ubongo wa mtoto huyo.
Mamake Cyprian, alikuwa miongoni mwa watu sita waliouawa katika shambulizi hilo, baada ya washukiwa watatu wa ugaidi kulivamia kanisa la Joy in Jesus katika mtaa wa Likoni na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholela.
Cyprian atafanyiwa upasuaji maalum katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi ambao utagharamiwa na serikali.www.newinfotz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment